Wasiliana Nasi

Washirika wa Elimu

Washirika wa elimu wa BRPHSC wanasaidia kuziba pengo kati ya elimu na ajira kwa kukuza uwezo wa kupata mafunzo ya sekta, vyeti na shahada kwa wanafunzi na walimu, kuunganisha wanafunzi na waajiri, kuwapa waajiri uwezo wa kupata wafanyakazi watarajiwa wa siku zijazo, na zaidi. 

Ushirikiano huu unahudumia eneo lote la GO Virginia Region 2 ambalo linajumuisha miji ya Covington, Lynchburg, Radford, Roanoke na Salem; na kaunti za Alleghany, Amherst, Appomattox, Bedford, Botetourt, Campbell, Craig, Floyd, Franklin, Giles, Montgomery, Pulaski na Roanoke. Tunakaribisha vitengo vyote vya usimamizi wa shule za chekechea na za msingi (K–12), vyuo vya jamii, taasisi za elimu ya vyuo vya shahada ya kwanza na taasisi za elimu ya juu katika eneo hili kuwa mshirika wa elimu. 

MALENGO YETU 

Viongozi wa BRPHSC wameunda mbinu ya mchanganyiko wa mafunzo ya umma na ya kibinafsi ambayo inatumia nyenzo zilizopo, kusanifisha mtaala wa kina ulioundwa na waajiri, na kuujumuisha ndani ya mfumo wa elimu kuanzia shule ya chekechea na za msingi (K-12) hadi viwango vya elimu ya baada ya shule ya sekondari. 

Baadhi ya malengo muhimu ya Ushirikiano huu yanajumuisha:  

  • Kuziba mapengo ya elimu kati ya vitengo vya usimamizi wa shule, vyuo vya jamii na taasisi za elimu ya vyuo vya shahada ya kwanza 
  • Kuhakikisha alama za mtaala husika zinaweza kuhamishiwa kati ya vyuo vya jamii na taasisi za elimu ya vyuo vya shahada ya kwanza 
  • Kukuza uwezo wa kupata mafunzo ya sekta, vyeti na shahada kwa wanafunzi na walimu 
  • Kuondoa vizuizi vya mafanikio ya mpango kwa kuongeza idadi ya walimu waliohitimu, kupanua nafasi za mafunzo ya kazi, na kushughulikia huduma za usaidizi wa wanafunzi
  • Kuhakikisha eneo lina wataalamu waliohitimu wa sayansi za afya ili kutimiza mahitaji ya waajiri wa huduma za afya wa eneo letu, kusaidia kuvutia na kudumisha kampuni zinazotafuta kuhamia katika eneo letu na kutimiza mahitaji ya wafanyakazi ya biashara mpya 

Washirika wa Sasa wa Elimu

Vitengo vyote vya Usimamizi wa Shule za chekechea na za msingi (K-12) na taasisi za mafunzo ya juu katika eneo la GO Virginia Region 2 zinakaribishwa kushiriki

Wadau Halisi

Ushirikiano wa Blue Ridge wa Kazi za Sayansi ya Afya (Blue Ridge Partnership for Health Science Careers) unatafuta washirika wapya kila wakati. Je, shirika lako linataka kuhusika? Wasiliana nasi kwa kutumia fomu iliyo hapa chini.

Anza kufanya kazi katika sekta ya Sayansi ya Afya.